Mvua kubwa kuendelea sehemu kadhaa za nchi

Maeneo yatakayopokea mvua kubwa ni pamoja na eneo la Ziwa Victoria, Magharibi, baadhi ya sehemu za nyanda za juu eneo la kati na mwambao wa pwani.

Tom Mathinji
1 Min Read
Mvua kuendelea kunyesha katika sehemu mbali mbali za nchi.

Sehemu kadhaa za humu nchini zitaendelea kushuhudia mvua kubwa, kulingana na Idara ya Utabiri wa Hali ya Hewa.

Idara hiyo imetoa tadhari hiyo ikisema maeneo mengi ya nchi yataendelea kupokea mvua kubwa hadi Machi 9, 2026.

Kwenye tahadhari hiyo, idara hiyo imedokeza kuwa  maeneo yatakayopokea mvua kubwa ni pamoja na eneo la Ziwa Victoria, Magharibi, baadhi ya sehemu za nyanda za juu eneo la kati na mwambao wa pwani.

Kutokana na hayo, wananchi wameonywa kuhusu uwezekano wa mafuriko na ukungu, huku wakionywa dhidi ya kuvuka au kuendesha magari katika sehemu zilizofurika.

Idara hiyo imesema msimu wa mvua ya masika umeanza mapema kuliko kawaida katika baadhi ya maeneo ya nchi, japo hali ya ukavu itashuhudiwa kuanzia katikakati mwa mwezi Machi katika baadhi ya sehemu za nchi.

Share This Article