Muungano wa Azimio la Umoja One Kenya, umesema utaandaa maandamano dhidi ya serikali Jumatano juma lijalo.
Katika mkutano na wanahabari siku ya Alhamisi, muungano huo ulitangaza siku tano za kuwaomboleza waandamanaji waliofariki jana Jumatano.
Muungano huo umeitisha maandamano ili kuishurutisha serikali kufanyia marekebisho sheria ya fedha ya mwaka 2023, ukizindiua zoezi la kukusanya saini milioni 15.
Kiongozi wa upinzani Raila Odinga, alisema ukusanyaji wa saini hizo, unalenga kuilazimisha serikali kuzingatia sheria.
Hadi kufikia sasa, muungano huo umesema umekusanya saini milioni 1.2 huku ukiwahimiza Wakenya kushiriki maandamano Jumatano juma lijalo.
Wakati wa uzinduzi wa tovuti ya kukusanya saini kidijitali ya www.tumechoka.com, Raila alisema ni kupitia umoja ndiposa serikali itasikiza malalamishi ya Wakenya.