Mutharika amwongoza Rais Chakwera uchaguzi mkuu Malawi

Dismas Otuke
1 Min Read
Peter Mutharika akipiga kura

Rais wa zamani wa Malawi Peter Mutharika, angali anaongoza kwenye kinyang’anyiro cha uchaguzi mkuu wa urais nchini Malawi dhidi ya Rais wa sasa Dkt. Lazurus Chakwera.

Kulingana na matokeo ya hivi punde yaliyotangazwa na mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini humo (MEC), Jaji Annabel Mtalimanja, Mutharika amepata kura 203, 440, dhidi ya Chakwera aliyezoa kura 153, 507.

Mtalinja ameahidi kutangaza matokeo rasmi ndani ya kipindi cha siku nane ambazo tume hiyo imetengewa kisheria.

Wapiga kura milioni 4.6 kati ya wapiga kura milioni 7.2 waliojisajili walijitokeza katika uchaguzi huo mkuu wa Septemba 16.

Hata hivyo, wadadisi wameashiria kuwa huenda mshindi akakosekana katika raundi ya kwanza na kulazimu kuandaliwa tena kwa raundi ya pili kubaini mshindi.

Website |  + posts
Share This Article