Museveni azindua ujenzi wa reli ya SGR nchini Uganda

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amezindua ujenzi wa reli ya kisasa ya Standard gauge railway (SGR) yenye uwezo wa kusafirisha mizigo tani 1,000 kwa wakati mmoja.

Reli hiyo ambayo ni ya kwanza nchini Uganda itachukua muda wa miezi 48 kukamilika,huku ikitizamiwa kubuni nafasi za ajira laki sita.

Akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa reli hiyo eneo la Tororo ,Museveni alisema ana imani kukamilishwa kwa muundo mbinu huo, kutaimarisha utalii na biashara kati ya Uganda na jirani zake Tanzania.

Fedha za ujenzi wa reli hiyo zinatolewa na benki ya Maendeleo barani Afrika na serikali ya Uganda.

Share This Article