Museveni apongeza NRM kwa kuafikiana kuhusu Spika na Naibu wake

Uchaguzi wa Spika na Naibu wake utaandaliwa leo Jumatatu katika bunge la Uganda.

Dismas Otuke
1 Min Read
Rais Museveni akiwa na Wabunge waliopendekezwa na NRM kuwa Spika na Naibu Spika.Picha hisani ya New Vision

Rais Yoweri Museveni wa Uganda amewapongeza wabunge wa chama tawala cha National Resistance Movement (NRM) kwa kuafikiana bila malumbano kuhusu viti vya Spika na Naibu wake.

Museveni alisema hayo mwishoni mwa juma alipokutana na wabunge wa NRM katika Ikulu ya Entebbe.

Rais Museveni alisisitiza umuhimu wa kutumia makubaliano katika kuwateua viongozi wa viti kama vya Spika na Naibu wake, badala ya kulumbana na kufanya kampeni kali ambazo huleta migawanyiko chamani.

Wabunge waliokuwa wakimezea mate viti hivyo walijiondoa na badala yake kuwapendekeza wenzao Jacob Oboth kuwa Spika na Thomas Tayebwa kuwa Naibu wake.

Uchaguzi wa Spika na Naibu wake utaandaliwa leo Jumatatu katika bunge la Uganda.

Share This Article