Museveni amsamehe Spika wa zamani Anita Annet Among

Mkuu wa majeshi Jenerali Muhoozi Kainerugaba alifichua haya kwenye mtandao wa X.

Marion Bosire
1 Min Read
Anita Annet Among

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amemsamehe Spika wa awali wa nchi hiyo Anita Annet Among na kuagiza Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini humo, Jenerali Muhoozi Kainerugaba, kumwachilia.

Haya yalifichuliwa na Kainerugaba kupitia mtandao wa kijamii wa X, hatua ambayo itafikisha kikomo kifungo cha nyumbani na vikwazo vilivyowekwa dhidi yake.

“Mzee pia amenielekeza nimuachilie AAA kutoka kifungo cha nyumbani,” Muhoozi alisema, akimrejelea Among kwa herufi za mwanzo za majina yake na kuongeza, “Tutafanya hivyo pia.”

Among alijiondoa katika kinyang’anyiro uspika wa Bunge la 12 kuruhusu uchunguzi kuhusu madai yaliyoibuliwa kumhusu yanayohusiana na rushwa, kutangaza mali na usimamizi wa fedha za Bunge.

Among amekuwa chini ya kifungo hicho cha nyumbani kwa zaidi ya siku 100 huku vyombo vya usalama vikichunguza madai yanayohusiana na rushwa na upatikanaji wa mali.

Wadhifa wa Spika kwa sasa unashikiliwa na Jacob Oboth Oboth, ambaye alichaguliwa kuongoza Bunge la 12.

Mtumizi mmoja wa mtandao wa X kwa jina Joshua Kamusiime aliuliza Kainerugaba iwapo mashtaka ya jinai dhidi ya Among yataendelea, lakini mkuu huyo wa jeshi alikana akisema kwamba babake Rais Museveni aliamua kumsamehe.

Share This Article