Museveni ajitolea kupatanisha Somaliland na Somalia

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni amejitolea kuongoza juhudi za kuleta upatanisho kati ya  Somalia na Somaliland.

Museveni ametangaza haya siku ya Ijumaa katika Ikulu ya Entebe alipokuatana na mjumbe maalum wa Somaliland Dkt Jama Musse Jama.

Museveni alikariri kujitolea kuinganisha pande hizo mbili akisema kamwe haungi mkono kujitenga kwa Somaliland kutoka kwa taifa la Somalia,akiwataka viongozi wa pande zote  mbili kuweka kando tofauti za kisiasa kwa minaajili ya maendeleo ya taifa .hilo

 

Share This Article