Kampuni ya Afrika Kusini ya Multichoice, iliadhimisha miaka 30 tangu kujiunga na tasnia ya runinga na filamu humu nchini .
Ili kushereherehelea miongo hiyo mitatu, Multichoice imeanzisha kampeini ya kuwatuza wateja wake ambayo itaandelea hadi Septemba 30 mwaka huu, kwa wateja wa huduma za DStv, Showmax, na GOtv.
Meneja Mkurugenzi wa Multichoice Kenya Nzola Miranda, alisema wamewekeza shilingi bilioni 6.5, tangu mwaka 2016 katika sekta ya filamu nchini ambazo zimewaajiri Wakenya wengi.
Sherehe hizo pia zilishuhudia waigizaji maarufu wa humu nchini na watayarishaji vipindi wakituzwa kwa jitihada za kuinua tasnia hiyo humu nchini.