Muhoozi mwanawe Museveni akana kuwania Urais mwaka ujao

Dismas Otuke
1 Min Read

Mwana wa kiume wa Rais wa Uganda Jenerali Muhoozi Kainerugaba amekanusha madai yaliyozagaa kuwa anapania kuwana Urais kumpinga babake katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2026.

Kainerubaga amekuwa mstari wa mbele wa kuwatia hamasa raia kujiandikisha kwa upagaji kura za mwaka ujao,huku wengi wakikisia kuwa alilenga kumpinga babake katika uchaguzi wa mwaka 2026.

Museveni aliye na umri wa miaka 80 wa chama cha Uganda People’s Democratic Front amekuwa uongozini kwa takriban miongo minne.

Kainerubaga alikuwa amebuni vuguvugu la Patriotic League Uganda (PLU) la kuwahamasisha wapiga kura wengi wakidhani kuwa alikuwa ajitose ulingoni kuvaana na babake.

Share This Article