Mudavadi: Kenya na Ujerumani zitaendelea kuimarisha uhusiano

Tom Mathinji
1 Min Read
Waziri mwenye Mamlaka Makuu Musalia Mudavadi.

Waziri mwenye Mamlaka Makuu Musalia Mudavadi, amesema Kenya itazidi kuimarisha ushirikiano kati yake na Ujerumani, hususan katika sekta ya biashara na uwekezaji.

Mudavadi ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje, alisema sehemu nyingine ambako nchi hizi mbili zitashirikiana ni pamoja na uhamiaji wa wafanyakazi,hatua za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya anga,elimu na afya.

Mudavadi aliyasema hayo leo Jumanne pembezoni mwa mkutano wa tano wa kibiashara kati ya Kenya na Ujerumani Jijini Nairobi, ambapo alisema Ujerumani imeahidi kupanua shughuli zake hapa nchini hasaa katika utengenezaji wa magari aina ya Volkswagen.

“Kujitolea kwa ujerumani katika kuongeza utengenezaji wa magari ya uchukuzi wa umma kwa ushirikiano na kampuni za hapa nchini, kutapiga jeki sekta ya viwanda katika kanda ya Afrika Mashariki,” alisema Mudavadi.

Waziri huyo alisema baada ya mazungumzo na maafisa wa kampuni ya kutengeneza magari ya Volkswagen, kampuni hiyo imetangaza kuwa itarejesha utengenezaji wa magari yake hapa nchini kufikia mwishoni mwa mwaka huu.

Alisema vijana wa bara la Afrika  ambao wanawakilisha asilimia 60 ya jumla ya idadi ya watu wa Afrika wana hamu ya kuwa wabunifu, kutumia teknololojia ya kisasa na kuimarisha hali ya baadaye ya bara hili.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *