Mudavadi, Duale na Mvurya kukaimu Wizara

Dismas Otuke
1 Min Read

Mkuu wa Utumishi wa Umma Felix Koskei  ametangaza kuwa Mawaziri Musalia Mudavadi, Aden Duale na Salim Mvurya wameongezewa majukumu serikalini.

Kwenye taarifa leo Jumamosi, Koskei ametangaza kuwa Mudavadi ambaye ni Kinara wa Mawaziri na pia Waziri wa Mambo ya Nje atahudumu kama kaimu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Uchumi wa Dijitali.

Duale ambaye ni Waziri wa Mazingira  ndiye kaimu Waziri wa Kilimo wakati Mvuyra akihudumu kama kaimu Waziri wa Biashara, Uwekezaji na Viwanda, wadhifa alioushikilia kabla ya kuhamishiwa kwenye Wizara ya Michezo katika mabadiliko yaliyofanywa na Rais William Ruto siku chache zilizopita.

Watatu hao watashikilia nyadhfa hizo kusubiri kamati ya bunge kuwapiga msasa Mawaziri watatu wateule ambao ni William Kabogo, Mutahi Kgawe na Lee Kinyanjui mwezi Januari mwakani.

Kabogo ameteuliwa kuwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Uchumi wa Dijitali, Kagwe ametwikwa jukumu la kuongoza Wizara ya Kilimo wakati Kinyanjui akiteuliwa kuwa Waziri wa Biashara, Uwekezaji na Viwanda.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *