Mudavadi atoa wito wa kuheshimiwa kwa taasisi huru

Tom Mathinji
1 Min Read

Waziri mwenye mamlaka makuu Musalia Mudavadi ametoa wito kwa wakenya kuheshimu uhuru wa taasisi mbalimbali, akisema taasisi hizo ni nguzo muhimu kwa uthabiti wa taifa hili.

Mudavadi alitaka kuheshimiwa kwa mfumo wa sheria, akidokeza kuwa taasisi huru zinapaswa kupewa fursa ya kutekeleza majukumu bila uwoga au mapendeleo.

“Tunapaswa kutekeleza kilicho sahihi kila wakati. Tunapaswa kudumisha uhuru wa taasisi mbali mbali ili ziwe thabiti, bila mapendeleo na za haki katika kuwatumikia wananchi,” alisema mudavadi.

Mudavadi aliyepia waziri wa mambo ya nje, aliyasema hayo leo Jumamosi wakati wa mazishi ya Mama Femina Khayisia, mamake mkurugenzi wa mashtaka ya umma Renson Ingonga, katika kijiji cha Makunga kaunti ya Kakamega.

Akizungumza katika mazishi hayo, spika wa bunge la taifa Moses Wetang’ula, aliwahimiza viongozi kuhakikisha taifa hili lina utulivu.

Wengine walioandamana na Mudavadi ni pamoja na mawaziri Moses Kuria na Aisha Jumwa, Magavana Fernandes Barasa, Johnson Sakaja, Jonathan Bii na Paul Otuoma.

Share This Article