Wanafunzi wa kidato cha nne kote nchini wameanza mtihani wa KCSE mapema leo Jumatatu kwa somo la Kiingereza, karatasi ya kwanza na somo la Kemia, karatasi ya kwanza.
Wanafunzi 903,260 wanakalia mtihani huo unaotarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi huu.
Kesho Jumanne, wanafunzi watafanya mtihani wa Hisabati na Kiingereza, karatasi ya pili.
Serikali imeimarisha usalama na ulinzi madhubuti wa mitihani kwa kuweka mikakati ya kukabiliana na changamoto za maeneo yenye utovu wa usalama na yaliyoathirika na mafuriko.
Aidha imeonya kuwa yeyote atakayepatikana akijihusisha katika visa vya wizi wa mtihani atachukuliwa hatua kali.