Msimu wa kuvuna macadamia kuanza kesho

Dismas Otuke
1 Min Read

Waziri wa Kilimo Mutahi Kagwe ametangaza kuanza kwa msimu wa kuvuna zao la macadamia Jumamosi hii Machi mosi.

Wakati uo huo Waziri Kagwe ametangaza kudumisha marufuku ya uuzaji nje ya nchi, njugu zote mbichi katika juhudi za kuhakikishia Kenya inafikia viwango vya kimataifa vilivyowekwa na mamlaka ya kilimo na chakula (FAO), na shirika la mazao ya mafuta za mwaka 2020.

Aidha, Kagwe amewataka wakulima wa macadamia nchini kujiandikisha kwenye mfumo jumuishi wa kilimo (KIAMIS), ili kuisaidia serikali, sekta ya kibinafsi, na wadau wengine kuratibu vyema mipango na sera za kuimarisha kilimo hicho nchini.

Kwenye mkutano wa jana kati ya waziri Kagwe na kamati iiliyowakilisha wakulima wa macadamia, aliagiza idara zote zikiongozwa na maafisa wa polisi, kuhakikisha sheria zinazothibiti zao hilo la macadamia zinazingatiwa ili kuhakikisa ni macadamia bora na zilizokomaa pekee zinavunwa na kuuzwa sokoni.

Website |  + posts
Share This Article