Msimu mpya wa Ligi Kuu Kenya kuanza Jumamosi

Dismas Otuke
1 Min Read

Msimu mpya wa Ligi Kuu Ya Kenya mwaka  2024/2025 utang’oa nanga Jumamosi Agosti 24, kwa jumla ya mechi nne huku nyingine tatu zikipigwa Jumapili.

Posta Rangers watafungua pazia kwa mechi dhidi ya Bandari FC katika uchanjaa wa Machakos kuanzia saa saba Adhuhuri,kabla ya kuwapisha wahifadhi hela Kenya Commercial Bank, watakogaragazana na Kariobangi Sharks kiwarani Police Sacco mida ya tisa alasiri.

Bidco United wataanza msimu nyumbani katika uwanja wa Manispaa wa Thika dhidi ya Shabana FC pia majira ya saa tisa na kisha Wagema Mvinyo Tusker FC ,wapambane dhidi ya Sofapaka uwanjani Machakos saa tisa.

Jumapili Agosti 25 Ulinzi Stars watakuwa nyumbani Ulinzi Complex kumenyana na Murang’a Seal,AFC Leopards iwazuru Mathare United waliopandishwa ngazi ,mechi hiyo ikisakatwa saa tisa katika uga wa Dandora .

Mabingwa wa National Super League Mara Sugar wataanza maisha ya Ligi Kuu kwa kuwaalika Kakamega Homeboyz  katika uwanja wa  Awendo saa tisa.

Share This Article