Msichana wa miaka kumi na moja ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tano kutoka mtaa wa Shikhambi, viungani mwa mji wa Kakamega, anadaiwa kujitia kitanzi kwa njia tatatishi.
Mwili wa Racheal Obayo ulipatikanaka ukining’inia chumbani kwake muda mfupi baada ya kushiriki chakula cha mchana pamoja na baadhi ya familia yake.
Nyanyake, Alice Obayo, amesema alipokea simu kuhusu kisa hiki alipokuwa ametoka nyumbani.
Anaseema mwendazake hakuwa na changamoto yoyote tangu utotoni na hakusikia malalamiko yoyote kutoka kwake.
Familia pamoja na viongozi wa nyumba kumi mtaa wa Shikhambi, akiwemo mzee wa nyumba kumi, Reuben Otiede, wanatoa wito kwa uchunguzi wa kina kufanywa ili kufahamu kiini cha kifo cha mwanafunzi huyo.
Mwili wa mwendazake umehifadhiwa katika makafani ya hospitali ya rufaa kakamega kwa uchunguzi zaidi.