Maafisa wa huduma ya taifa ya polisi wakishirikiana na asasi zingine za usalama, wamemkamata mshukiwa wa wizi wa shilingi 500,000, ulioripotiwa katika kituo cha polisi cha Wamba siku ya Jumatatu.
Felix Ayiera alitiwa nguvuni katika eneo la Kalama kwenye barabara kuu ya Isiolo-Marsabit.
Mshukiwa huyo alikamatwa akiwa ameabiri gari aina ya Probox, akiwa na shilingi 497,350.
kulingana na maafisa wa upelelezi wa maswala ya Jinai DCI wa Samburu Mashariki, walianzisha uchunguzi baada ya mfanyabiashara kuripoti kuwa fedha zake zilitoweka katika hoteli anakohudumu.
Aidha mfanyabiashara huyo alidai kuwa alipoteza shilingi 500,000 katika biashara yake, na kwamba mshukiwa mkuu Felix Ayiera alikuwa hajulikani aliko huku simu yake ya rununu ikiwa imezimwa.