Mshukiwa wa ujambazi akamatwa katika kaunti ya Kakamega

Marion Bosire
1 Min Read

Maafisa wa polisi katika eneo bunge la Malava kaunti ya Kakamega wanamzuilia mshukiwa mmoja sugu wa uhalifu katika eneo hili baada ya kumnasa na bastola na vifaa butu gua kutekeleza wizi.

Mshukiwa huyo alipatikana na silaha hatari zikiwemo bastola mbili aina ya ceska pamoja na sare na vifaa tofauti vya polisi.

Mkuu wa polisi katika eneo la Malava Paul Mwenda amesema maafisa wa polisi pamoja na maafisa wa DCI walimfumania mshukiwa Jackson Mwangi mwenye umri wa Miaka 38 akiwa mafichoni viungani mwa mji wa Malava baada ya kupokea ripoti kutoka kwa wananchi.

Mhalifu huyo anadaiwa kuwa mmoja wa wanachama wa genge hatari la majambazi ambalo limekuwa likitekeleza misururu ya visa vya uhalifu eneo hilo.

Share This Article