Mshukiwa wa shambulizi lililotokea kwenye dhifa ya wanahabari iliyoandaliwa na Rais wa Marekani Donald Trump, ameshtakiwa kwa jaribio la mauaji.
Cole Tomas Allen mwenye umri wa miaka 31, pia alishitakiwa kwa makosa mengine mawili kwa kupatikana na silaha alipofikishwa mbele ya mahakama mjini Washington DC siku ya Jumatatu.
Kulinganana viongozi wa mashtaka, Tomas alipatikana na bunduki mbili na visu vitatu alipokuwa akipita eneo la ukaguzi wa usalama wakati wa dhifa ya wanahabari katika Ikulu ya White House siku ya Jumamosi.
Aidha, aliifahamisha mahakama alikuwa na shahada ya uzamili, huku wachunguzi wakisema mwanamume huyo alitaka kuwaua maafisa wengi iwezekanavyo wa ngazi ya juu.
Wakati wa tukio la Jumamosi usiku, Trump, Makamu wa Rais JD Vance, wajumbe wa Baraza la Mawaziri na maafisa wengine wa Ikulu ya White House, waliondolewa kwenye ukumbi wa hoteli ya Washington Hilton baada ya milio ya risasi kusikika.