Mshukiwa mkuu wa uhalifu atiwa nguvuni kaunti ya Meru

Tom Mathinji
1 Min Read
Mhalifu akamatwa akiwa na silaha kaunti ya Meru.

Maafisa wa polisi wamemtia nguvuni mshukiwa mkuu anayehusishwa na misururu ya uhalifu katika eneo la Buuri Mashariki kaunti ya Meru.

Fredrick John Mwenda, alikamatwa na maafisa wa idara ya kukabiliana na makosa ya jinai(DCI), wakishirikiana na maafisa wa polisi wa kituo cha polisi cha Kathare, baada ya kupokea habari kutoka kwa wananchi.

Mshukiwa huyo alitiwa nguvuni baada ya maafisa hao kutekeleza operesheni katika maficho ya mshukiwa huyo yaliyoko katika kijiji cha Maili Tano, kata ya Ruiri Rwarera.

“Baada ya ukaguzi wa kina katika makazi ya mshukiwa huyo, maafisa wa polisi walipata bunduki yenye nambari za usajili 001422, ikiwa haina sehemu yake ya nyuma,” ilisema idara ya DCI kupitia ukurasa wake wa twitter.

Wakati wa operesheni hiyo, maafisa hao pia walipata risasi 18, na kifaa cha kuweka risasi kilichokuwa kimefungwa kutumia karatasi ya plastiki.

Mwenda kwa sasa anazuiliwa katika kituo cha polisi akisubiri kufikishwa mahakamani.

Website |  + posts
TAGGED:
Share This Article