Wapasuaji wa mbao kutoka kaskazini mwa Bonde la Ufa wameitaka serikali kuwaruhusu kuvuna miti waliokuwa wamenunua kutoka kwa serikali.
Wakizungumza na wanahabari, wapasuaji hao wamesema kuwa miti yao inaendelea kuozea msituni kutokana na marufuku iliyowekwa na serikali tangu mwaka 2018.
Wakiongozwa na Benjamin Kuto, wanasema wengi wao wamehangaishwa na benki za kutoa mikopo kwani walichukua mikopo kulipia miti hiyo ya serikali.
Wapasuaji mbao hao hata hivyo wameahidi kufanya kampeni ya kupanda miche takriban milioni 2 kwenye misitu mbalimbali katika eneo hilo.
Wengine waliokuwapo wakati wa mkutano na wanahabari ni Morgan Kennedy Avugwe na David Njogu ambao ni wapasua mbao na mfanyabiashara Chelegat Thomas.