Mshukiwa anayejisingizia kuwa afisa wa EACC akamatwa

Tom Mathinji
1 Min Read
Mshukiwa akamatwa kwa kujisingizia kuwa afisa wa tume ya EACC.

Maafisa wa tume ya Maadili na kukabiliana na ufisadi EACC, wamemtia nguvuni mshukiwa anayejisingizia kuwa wakili wa kukabiliana na ufisadi na mchunguzi, anayedaiwa kuwatapeli maafisa wa serikali, wanakandarasi, wasambazaji bidhaa na wananchi kwa jumla.

Akithibitisha kukamatwa kwake, msemaji wa EACC  Eric Ngumbi, alidokeza kuwa tapeli huyo Ezely Omwoyo, amekuwa akiwahadaa waathiriwa kuwa yeye ni mchunguzi wa tume ya EACC, ambaye yuko katika harakati za kukamilisha uchunguzi wa kesi za ufisadi dhidi yao.

Mshukiwa huyo huwaeleza wathiriwa kuwa watatiwa nguvuni, lakini ana uwezo wa kuwaondoa mashakani na kufutilia mbali kesi za ufisadi dhidi yao iwapo watampa fedha alizokuwa akiitisha ambazo huwa ni mamilioni ya pesa.

Katika masikizano yake, yeye husema fedha hizo lazime ziwe zinatosha ili aweze kuwapa wakubwa wake na pia maafisa katika afisi ya kiongozi wa mashtaka na katika mahakama ya kukabiliana na ufisadi.

Mshukiwa huyo alikamatwa Alhamisi na kuzuiliwa katika kituo cha polisi kilichoko katika makao makuu ya tume ya EACC.

Anakabiliwa na mashtaka ya kujisingizia kuwa afisa wa EACC kinyume na kifungu cha 34(1) na kile cha 34(2) vya sheria za kukabiliana na ufisadi na uhalifu wa kiuchumi.

TAGGED:
Share This Article