Msanii kutoka Uganda aeneza sifa za Afrika nchini China kupitia uchongaji vinyago.

Tom Mathinji
2 Min Read

Joseph ni mchongaji vinyago kutoka Uganda. Mwaka huu, ni mara yake ya pili kufanya kazi nchini China. Ametengeneza mamia ya vinyago kwa kutumia mbao katika bustani la kiafrika la Changsha. 

Kando na kutambua ndoto yake ya uchongaji vinyago, ametangamana na watu wengi ambao wamepata fursa ya kuelewa zaidi ubora wa Afrika. Hii hapa hadithi yake.

Mwaka wa 2023, niliishi katika mji wa Changsha nchini China, ambapo nilichonga vinyago vingi.

Kulikuwa na shindano nchini Uganda. Niliteuliwa bora zaidi miongoni mwa washindani. Kwa hivyo niliteuliwa na serikali.

Mimi ni msanii kutoka Afrika. Nitaeneza urembo na nguvu ya Afrika, ili watu wengi wajue uzuri wa Afrika.

Nilitengeneza huyu tembo kuonyesha kuwa huyu ni tembo wa kiafrika. Kwa hivyo tunataka kuonyesha ulimwengu Afrika ina nini, kwa kuchonga vinyago.

Kwanza kabisa, bustani hii imetusaidia kuelewa zaidi China. Tumepelekwa kwenye ziara za nje mara nyingi. Tumeenda katika miji tofauti ili kusoma mengi kuhusu China.

Tulitengeneza kiti hiki, ambacho asili yake ni Afrika. Tulipata malighafi kutoka hapa China.

Kwa hivyo hii bidhaa tuliyoitengeza kutoka kwa mbao ya China, na ni kiti cha Kiafrika.

Ni tamu sana…..Kwa sasa, nimeongeza mwili kutokana na chakula ninachopewa.

Watu ni wachangamfu na wangwana. Wana ucheshi mwingi.

Kwa hivyo, nimepata uzoefu mwingi sana kwa kutangamana, nimeendeleza ujuzi wangu, nimepata maarifa ya kuendeleza uundaji wa bidhaa zangu, kando na kujionea bidhaa mpya.

Kama hii…

Bado tunajifunza Kichina. Ijapokuwa ni kigumu kiasi, tunajitahidi kujifunza. Hii itatusaidia kuwa karibu na wenyeji wa hapa na kufanikisha mawasiliano kati yetu kwa haraka.

Nilipewa zawadi kadhaa. Zipo hapa kwenye begi langu…..hivi ni viatu…televisheni.

Nitatumia uzoefu wangu na hadithi zangu kuonyesha ulimwengu kwamba Waafrika wana nguvu na uwezo wa kuchapa kazi.

Nitawaelezea wenzangu kule Afrika hadithi yangu ya China

Share This Article