Mratibu wa mpango wa IFAD nchini Kenya Ronald Ajengo akizuru mradi wa kuimarisha nafaka nchini Kenya (KCEP-CRAL) katika Kaunti ya Kilifi anasema mradi huo unaotekelezwa katika kaunti 13 unalenga kupunguza umaskini na ukosefu wa chakula miongoni mwa wakulima wadogo katika sehemu kame nchini Kenya.
Mpango huo pia unalenga kuendeleza uwezo wao wa kiuchumi kwa kuboresha uwezo wao wa usimamizi wa maliasili na kustahimili mabadiliko ya hali ya hewa katika mfumo ikolojia unaozidi kuwa tete.
Wakulima wadogo elfu 14, wamefikiwa na mpango huo ambapo wamefunzwa mbinu za kilimo zenye mwelekeo wa kibiashara, zinazostahimili hali ya hewa kupitia uboreshaji wa rasilimali, mbinu za usimamizi baada ya uzalishaji na kuwaunganisha na soko.
Mradi huo pia unathamini serikali za kaunti na jamii ili kusimamia rasilimali zao kwa uendelevu kwa kujenga uwezo wao kustahimili mabadiliko ya hali ya hewa.
Mchanganuzi wa maswala ya mazingira na tabianchi katika IFAD Clemence Monier anasema faida za ustahimilivu wa mabadiliko ya tabianchi ni za muda mfupi na muda mrefu na zinahusu utunzaji wa mfumo ikolojia ili kupambana na majanga kama mafuriko.
Norah Zanzua mmoja wa wanaofaidika na mpango huo anasema kwamba wasichana na kina mama ambao walikuwa wakitembea mwendo mrefu kupata maji sasa wanafurahia.
Wasichana wanaweza kuendelea na masomo bila shida hatua iliyopunguza wanaoacha masomo ikifananishwa na wenzao wa kiume.