Moto wazuka huku milipuko ikisikika katika duka la gesi Ngara

Marion Bosire
1 Min Read

Wakazi wa eneo la Ngara karibu na jiji la Nairobi leo waliamshwa na mlipuko mkubwa na moto mkubwa katika duka la kuuza mitungi ya gesi katika barabara ya Desai.

Ripoti za mwanzo zinaashiria kwamba moto ulianza kabla ya mlipuko na baadaye moto huo ukasambaa kwenye duka zilizo karibu pamoja na majengo.

Video zinazosambazwa mtandaoni zinaonyesha kwamba moto huo wa alfajiri uliendelea kwa muda kabla ya wazima moto na maafisa wa polisi kufika kudhibiti hali.

Wakenya mitandaoni wameshtuliwa na tukio hilo lililojiri miezi michache baada ya tukio jingine sawa na hilo katika eneo la Embakasi kaunti ya Nairobi.

Hakuna ripoti zilizotolewa kufikia sasa kuhusu majeruhi kwenye kisa cha leo hata ingawa magari ya ambulensi yalionekana katika eneo hilo.

Chanzo cha moto pia hakijabainika.

Share This Article