Moto wateketeza nyumba huko Donholm Nairobi

Marion Bosire
1 Min Read

Moto umeteketeza nyumba ya orofa mbili ya makazi katika barabara ya Manyanja eneo la Donholm jijini Nairobi.

Wapangaji wa nyumba za orofa hiyo waliweza kuokoa sehemu ya mali yao na hakuna majeruhi wala maafa yaliyoripotiwa kutokana na mkasa huo.

Wahudumu wa zima moto wanaendeleza juhudi za kuzima moto huo ambao tayari umechoma kabisa orofa ya juu kabisa. Kilichosababisha moto huo bado hakijajulikana.

Wakazi wa eneo hilo hata hivyo walilalamika kwamba gari ya kwanza ya zima moto iliyowasili katika eneo hilo haikuwa na maji na ya pili ndiyo ilikuwa na maji.

Mkasa huo ulisababisha msongamano wa magari kwenye barabara ya Manyanja hatua iliyolazimu polisi wa trafiki kuelekeza waendesha magari hadi barabara ya Outering.

Share This Article