Morocco watia kibindoni shilingi milioni 450 kwa kutwaa CHAN

Simba wa Atlas waliibwaga Madagascar magoli 3-2 katika fainali ya kusisimua iliyopigwa katika uchanjaa wa Kasarani Jumamosi jioni.

Dismas Otuke
1 Min Read

Morocco watatuzwa shilingi milioni 452 kwa kutwaa kombe la CHAN katika makala ya nane yaliyokamilika jana katika uwanja wa kimataifa wa Kasarani.

Simba wa Atlas waliibwaga Madagascar magoli 3-2 katika fainali ya kusisimua iliyopigwa katika uchanjaa wa Kasarani Jumamosi jioni.

Madagascar watapokea shilingi milioni 155 kwa kumaliza nafasi ya  pili wakati ,Senegal walioridhia nafasi ya tatu wakitia mkobani shilingi milioni 90.

Sudan iliyochukua nafasi ya nne itapokea shilingi milioni 77, wakati Kenya,Tanzania na Uganda waliofika kwota fainali wakituzwa shilingi milioni 58 kila moja.

Kindumbwendumbwe hicho kilikamilika jana huku mataifa 19 yakishiriki.

Website |  + posts
Share This Article