Morocco, Uhispania na Ureno ndio watakuwa waandalizi wa fainali za kombe la dunia za mwaka 2030.
Uamuzi huo umeafikiwa Jumatano jioni na baraza kuu la shirikisho la soka duniani FIFA .
Kulingana na FIFA kama nji moja ya kusherehekea karne moja tangu kaunzishwa kwa kipute cha kombe la dunia mwaka 1930 nchini Uruguay,mechi tatu za ufunguzi za kombe la dunia mwaka 2030 zitaandaliwa katika mataifa ya Uruguay,Paraguay na Argentina.
Itakuwa mara ya pili kwa nchi ya Afrika kuandaa fainali za kombe la dunia baada ya Afrika Kusini kuwa mwenyeji wa makala ya mwaka 2010.
FIFA imetangaza kuwa mataifa matatu ya Morocco,Uhispania na Ureno yanafuzu moja kwa moja kwa fainali za mwaka 2030 wakiwa wenyeji wa kindumbwendumbwe hicho.
Fainali za mwaka 2030 zitashirikisha mataifa 48