Bingwa wa Dunia katika mbio za mita 800 Mary Moraa amefyatuka na kusajili muda wa kasi huku akitwaa ushindi katika fainali ya mita 400,katika siku ya pili na ya mwisho ya mashindano ya uwanjani yaliyoandaliwa ugani Nyayo.
Moraa ambaye ni wa Polisi alichomoka na kuwaacha wenzake zikisalia mita 100 na kukata utepe kwa sekunde 54.96.
Moraa ambaye pia ni bingwa wa Jumuiya ya Madola amesema ametumia shindano hilo kutafuta kasi anapoanza msimu.
“Sijaridhika na muda ambao nimekimbia ,nilizungumza na kocha wangu nikamwomba aniruhusu nikishiriki mita 400, ili nitafute kasi .”akasema Moraa
Millicent Ndoro pia wa Police alichukua nafasi ya pili kwa sekunde 52.74, huku Damris Mutunga akiridhia nafasi ya tatu.
Wanariadha wengi walitumia mkondo huo kutafuta kasi na kujiandaa kwa majaribio ya kitaifa ya michezo ya Afrika, yatakayoandaliwa uwanja wa Nyayo mwezi ujao