Kocha wa timu ya taifa ya Morocco kwa chipukizi chini ya umri wa miaka 20, Mohamed OUAHBI, amekabidhiwa majukumu ya timu ya taifa ya Atlas Lions, inayojiandaa kwa fainali za Kombe la Dunia.
Ouahbi I aliye na umri wa miaka 49,anatawaa ukufunzi wa Simba wa Atlas kutoka kwa Walid Regraqui ambaye amekuwa usukani tangu mwaka 2022, akiwaongoza hadi nusu fainali ya Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza.
Ouahbi aliiongoza Morocco kutwaa Kombe la Dunia kwa vijana chini ya umri wa miaka 20 mwaka uliopita nchini Chile.
Aidha, shiriksiho la kandanda nchini Morocco (FRMF) limemteua Mreno João Sacramento, kuwa mmoja wa wakufunzi wa timu ya taifa.
Kulingana na Rais wa shirikisho la soka nchini Morocco FRMF, Fouzi Lekjaa, uteuzi huo unaiandaa Morocco kwa fainali za Kombe la Dunia mwaka 2030 zitakazoandaliwa kwa pamoja na Morocco, Uhispania na Ureno.
Morocco imejumuisha kundi C katika Kombe la Dunia mwaka huu pamoja na mabingwa mara tano Brazil,Haiti na Scotland.