Mlindalango David De Gea aondoka Manchester United

Tom Mathinji
1 Min Read
David De Gea. Picha/Hisani

Baada ya miaka 12 katika uwanja wa Old Trafford, mlindalango David de Gea ametangaza kuiaga timu ya Manchester United, inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini Uingereza.

De Gea mwenye umri wa miaka 32 na ambaye kandarasi yake ilitamatika mwezi Juni, alisema sasa yuko tayari kukabiliana na changamoto mpya.

De Gea alianza soka akiwa Atletico Madrid, kabla ya kujiunga na Manchester United mwaka 2011 na kuichezea mechi 545.

“Nilitaka kutuma ujumbe huu wa kuwaaga mashabiki wote wa Manchester United,” aliandika mchezaji huyo katika chapisho la mtandao wa kijamii.

Aidha aliwashukuru mashabiki wa Man U, akidokeza kuwa wameafikia mengi akiwa katika kilabu hicho cha nchini Uingereza.

“Natoa shukrani kwa upendo wa miaka 12 iliyopita. Tumefanikiwa mengi tangu Sir Alex Ferguson aliponileta katika klabu hii,” alisema De Gea.

“Kimekuwa kipindi kisichosahaulika na chenye mafanikio tangu nilipokuja hapa. Sikufikiria kutoka Madrid nikiwa kijana mdogo tungefikia kile tulichofanya pamoja.

“Sasa, ni wakati mwafaka wa kuchukua changamoto mpya, kujisukuma tena katika mazingira mapya.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *