Mlanguzi wa mihadarati atiwa nguvuni Mombasa

Tom Mathinji
1 Min Read
Magunia 16 ya bangi yanaswa Mombasa.

Mshukiwa wa ulanguzi wa mihadarati amekamatwa akiwa na kilo 864.9 za bangi, katika mtaa wa Green, eneo la kiembeni, kaunti ya Mombasa.

Kulingana na ripoti kutoka kituo cha polisi cha Kadzandani, maafisa wa polisi walipata habari za kijasusi, kumhusu mlanguzi huyo aliyekuwa akitekeleza shughuli hiyo haramu katika eneo hilo.

Walipofika katika nyumba yake, maafisa hao wa polisi walipata magunia 16 ya bangi, yenye thamani ya shilingi milioni 25.

Mke wa mshukiwa huyo aliyetambuliwa kama Cynthia Anyango, pia alitiwa nguvuni na anawasaidia maafisa wa polisi kwa uchunguzi.

Bangi hiyo inazuiliwa na maafisa wa kitengo cha kukabiliana na mihadarati, mjini Mombasa.

TAGGED:
Share This Article