Mkwaju wa penalti waipa Man United ushindi dhidi ya Nottingham Forest

Francis Ngala
1 Min Read
Bruno Fernandes alifunga bao moja na kusaidia moja: Photo/ESPN

Manchester United ilipata ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Nottingham Forest nyumbani Old Trafford licha ya kutoboka mabao mawili ndani ya dakika 4 katika kipindi cha kwanza. 

Mabao ya mapema kutoka kwa mshambuliaji Taiwo Awoniyi raia wa Nigeria na Willy Boly katika dakika za mapema za mchezo kulikuwa kumewapa Nottingham Forest imani ya kutwaa ushindi wa kwanza wa ligi ugenini kwa mara ya kwanza kutoka Januari lakini tumaini hilo halikumea kwa muda kwani Christian Eriksen alipachika moja naye Casemiro akasawazisha mambo Old Trafford katika kipindi cha Pili.

Wachezaji wa Man United wakisherehekea ushindi wa 3-2 dhidi ya Nottingham Forest: Picha – Man United

Manchester United ilikuwa bora uwanjani na ilimiki mpira kwa kiwango kikubwa japo Forest walikuwa tishio katika mipira mirefu ya kuwatafuta safu ya ushambulizi yao ambayo ilikuwa imara katika kumalizia.

Nottingham Forest walipata pigo baada ya beki Joe Worrall kuonyeshwa kadi nyekundu katika kipindi cha pili, hali iliyowayumbisha katika eneo la ulinzi.

Bruno Fernandes alifunga bao la ushindi kupitia mkwaju wa penalti baada ya Marcus Rashford kuchezewa visivyo ndani ya eneo hatari.

Ushindi wa Man United ni wa pili katika mechi tatu walizocheza msimu huu.

 

 

Share This Article
Follow:
I am Versatile Multimedia Journalist with years of experience in Digital platforms, Live TV and Radio. In another world am a News Anchor and Reporter.