Mkuu wa Majeshi ya Uganda asema vikosi vya nchi hiyo vimepelekwa mjini Juba

Martin Mwanje
1 Min Read
Muhoozi Kainerugaba - Mkuu wa Majeshi ya Uganda

Mkuu wa majeshi ya Uganda Muhoozi Kainerugaba amesema vikosi maalum vya nchi hiyo vimepelekwa katika mji mkuu wa Sudan Kusini, Juba. 

Hatua hiyo inafuatia wasiwasi unaongezeka ambao umetishia makubaliano dhaifu ya amani.

Sudan Kusini imekumbwa na ukosefu wa kisiasia na usalama kwa muda mrefu, lakini hofu imeongezeka mno wiki moja iliyopita baada ya machafuko kuzuka kati ya vikosi vinavyounga mkono viongozi kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

“Siku mbili zilizopita, Vikosi vyetu Maalum viliingia mji wa Juba ili kuulinda,” alisema Kainerugaba kupitia mtandao wa X.

“Tutalinda eneo lote la Sudan Kusini kana kwamba ni letu,” alisema mwanawe Rais wa Yoweri Museveni na anayefahamika kwa kuweka ujumbe tata kwenye mtandao wa X.

Msemaji wa jeshi la Uganda Felix Kulayigye alithibitisha kuwa vikosi vya nchi hiyo vimepelekwa mjini Juba “ili kuilinda serikali”.

“Tulikuwa na maagizo ya kuvipeleka na tulipeleka vikosi hivyo huko,” aliiambia AFP.

Aliongeza kuwa vikosi hivyo vilipelekwa mjini humo siku mbili zilizopita.

Uganda ilituma vikosi nchini Sudan Kusini mnamo mwaka wa 2013 mwanzoni mwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka mitano ili kuunga mkono Rais wa sasa Salva Kiir, kabla ya kuondoka mwishoni mwa mwaka 2015.

 

TAGGED:
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *