Mkuu wa majeshi majeshi Francis Ogolla aliyefariki Alhamisi atazikwa Jumapili hii April 21 nyumbani kwake Alego Usonga katika kaunti ya Siaya.
Kulingana na ripoti rasmi kutoka kwa familia, mazishi yataandaliwa saa 72 baada ya kifo cha Ogolla kulingana na matakwa yake .
Ogolla atazikwa nyumbani kwake Mor, Alego kaunti Siaya .
Mazishi hayo yatatanguliwa na ibada katika kanisa lake la eneo la Nduri.
Mshirikishi wa mipango ya mazishi Joel Ogolla ,kutakuwa na ibada maalum ya kumbukumbuka marehemu tarehe 26 mwezi huu katika uwanja wa Ulinzi Sports Complex eneo la Langata.
Marehemu Ogolla alifariki baada ya ndege aliyokuwa akisafiria kuanguka katika eneo la Marakwet.