Mkutano wa sekta ya sukari kufanyika Kakamega Septemba

Martin Mwanje
1 Min Read

Kaunti 14 zinazopanda miwa zitafanya mkutano mjini Kakamega mwezi ujao kuangazia masaibu yanayoikumba sekta ya sukari nchini.

Huo utakuwa mkutano wa kwanza wa aina hiyo kuwahi kuandaliwa.

Gavana wa kaunti ya Kakamega Fernandes Barasa wakati akitoa tangazo hilo alidokeza kuwa mkutano huo unalenga kubuni mapendekezo yatakayosababisha kuwekwa kwa miundombinu na kutekelezwa kwa mabadiliko ya kudumu katika sekta ya sukari nchini.

Barasa aliyasema hayo jana Alhamisi wakati wa kusainiwa kwa kandarasi za utendakazi za mawaziri wa kaunti hiyo.

Alisisitiza haja ya kuilanisha sekta ya sukari nchini wakati huu ambapo usagaji miwa umesitishwa kwa kipindi cha miezi minne ijayo.

Alitaja kampuni za sukari kama vile Mumias zilizopo katika ukanda wa kiuchumi wa kanda ya Ziwa akisema zimekuwa zikisuasua katika utendakazi wake katika kipindi cha miezi michache iliyopita.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *