Mbunge wa Kigamboni nchini Tanzania, Dkt. Faustine Ndugulile amefariki dunia,usiku wa kuamkia leo tarehe 27 Novemba, 2024 akipatiwa matibabu nchini India.
Taarifa ya kifo chake imethibitishwa na Spika wa Bunge la Taifa Dkt. Tulia Ackson ambaye amemtaja mbunge huyo kuwa kielelezo kwa watanzania wote.
“Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Mbunge wa Kigamboni na Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Kanda ya Afrika, Mheshimiwa Dkt. Faustine Ndugulile, kwa niaba ya Wabunge natoa pole kwa Familia, Wakazi wa Kigamboni na Watanzania wote, Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi” akasema Tulia.
Spika wa bunge Tulia Ackson amesema ofisi ya bunge kwa ushirikiano na Familia inaendelea kuratibu shughuli za mazishi na taarifa zaidi zitaendelela kutolewa, “Bwana ametoa na Bwana ametwaa, apumzike kwa amani” Tulia akasema.
Dkt. Ndugulile alikuwa Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Kanda ya Afrika, ambaye alipaswa kuanza majukumu hayo mapya Februari mwakani (2025).
I am Versatile Multimedia Journalist with years of experience in Digital platforms, Live TV and Radio. In another world am a News Anchor and Reporter.