Mitihani wa KCSE waanza kote nchini

Tom Mathinji
1 Min Read

Mtihani wa mwaka huu wa kitaifa wa kidato cha nne KSCE, umeanza leo Jumanne, huku watahimiwa 965,501wakitarajiwa kufanya.

Mitihani huo utaandaliwa katika vituo 10,755 kote nchini.

Wanafunzi hao wataanza na Mitihani ya lugha ya Kifaransa, Kijerumani, Lugha ya Ishara, Kiarabu, Muziki na Sayansi ya nyumbani.

Shule zinatarajiwa kufungwa kuanzia wiki hii kwa likizo ndefu ya mwisho wa mwaka.

Kulingana na Baraza la Kitaifa la mitihani hapa nchini, mitihani ya Kitaifa ya mwaka huu, itaandaliwa kati ya Oktoba 22, hadi Novemba 22.

Ili kufanikisha usambazaji wa mitihani hiyo, Baraza hilo la limeongeza vituo vingine 41 na kufikisha jumla ya vituo 617 vya kusambazia mitihani nchini.

Katibu mkuu wa chama cha kitaifa cha walimu nchini-KNUT Collins Oyuu jana aliwataka wakaguzi kuhakikisha mitihani hiyo inasimamiwa vyema.

TAGGED:
Share This Article