Mimi Mars aondoka hospitalini

Marion Bosire
1 Min Read

Mwanamuziki na mwigizaji wa Tanzania Mimi Mars hatimaye ameondoka hospitalini na hali yake inaripotiwa kuendelea kuimarika.

Mars ambaye jina lake halisi ni Marianne Namshali Mdee aliruhusiwa kuondoka hospitalini alikokuwa amelazwa kufuatia ajali ya gari aliyopata zaidi ya wiki mbili zilizopita.

Dadake Mars, Vanessa Mdee ambaye anaishi nchini Marekani alimzuru kwa muda mfupi nchini Tanzania na alichapisha video fupi inayowaonyesha wakiwa katika wadi hospitalini.

Ajali hiyo ilipotokea, wengi walianza kukisia mitandaoni kwamba Mars alikuwa katika hali mbaya wengine wakidhania kwamba aliaga lakini ameimarika na sasa anaweza hata kuzungumza.

Inasemekana kwamba madaktari wamemzuia kutumia simu yake ya mkononi.

Share This Article