Mikwangurano ya kufuzu AFCON mwakani kupigwa Jumamosi

Dismas Otuke
1 Min Read

Jumla ya michuano saba ya raundi ya tano hatua ya makundi, kufuzu kwa fainali za kombe la AFCON mwaka ujao nchini Ivory Coast itapigwa Jumamosi.

Katika kundi H Chipolopolo ya Zambia watawaalika wenyeji wa kipute hicho Ivory Coast nao Lesotho wamenyane nyumbani dhidi ya Comoros katika pambano jingine kundini.

Palancas Negras ya Angola itakuwa ugenini dhidi ya Jamhuri ya Afrika ya kati, katika kundi E.

Equatorial Guinea watakuwa nyumbani kuvaana na Carthage Eagles ya Tunisia ambao tayari wamewahi tiketi katika kundi J,huku Libya na Botswana wakipimana ubabe katika mechi ya pili ya kundi hilo.

Kivumbi kinatarajiwa kule Johannesburg wakati wenyeji Bafanabafana watawatumbuiza miamba Morocco ukipenda Atlas Lions, katika mchuano pekee wa kundi K.

Afrika Kusini na Morocco tayari wamejikatia tiketi kushiriki dimba la AFCON mwaka ujao.

Mabingwa watetezi Senegal almaarufu Teranga Lions watawatembelea Benin katika kundi L.

Simba wa Teranga tayari wamefuzu kutetea kombe hilo.

Mataifa manane yamejikatia tiketi kwa kipute hicho kitakachoandaliwa kati ya Januari 13 na Februari 11 mwaka ujao nchini Ivory Coast.

Timu zilizofuzu ni wenyeji Ivory Coast, Tunisia,Algeria,Misri,Morocco,Afrika Kusini,Burkina Faso na Senegal .

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *