Mike Johnson achaguliwa tena Spika wa bunge la uwakilishi Marekani

Dismas Otuke
1 Min Read

Bunge la Congress nchini Marekani limemchagua tena Mike Johnson wa chama cha Republican kuwa Spika katika uchaguzi uliokuwa na ushindani mkali siku ya Ijumaa.

Johnson alishindwa kupata wingi wa kura unaohitajika katika raundi ya kwanza ili kutangazwa mshindi na baada ya mashauriano ya zaidi ya saa mbili ,Johnson alipata kura 219 dhidi ya 215 za Democrats na kutangazwa mshindi.

Uchaguzi wa jana ulikuwa mtihani mkubwa wa kwanza kwa serikali ya Rais mteule Donald Trump, huku baadhi ya Wabunge wa chama chake cha Republican wakionekana kumpinga hadharani.

Johnson amekuwa Spika baada ya kubanduliwa kwa mtangulizi wake Kevin McCarthy katikati ya muhula uliopita.

Spika huyo aliapishwa kuongoza kikao cha 119 cha bunge la Congress.

Chama cha Republican kinajivunia wabunge 53 dhidi ya 47 wa chama cha Democrat.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *