Migori na Siaya kuwania nafasi ya tatu Owalo Super Cup Alhamisi

Dismas Otuke
1 Min Read

Migori Combined na Siaya Combined zitashuka uwanjani siku ya Alhamisi kuwania nafasi ya tatu na nne katika makala ya kwanza ya michuano ya kuwania kombe la Eliud Owalo Super Super.

Mchuano huo utang’oa nanga saa sita Adhuhuri, kabla ya kupisha mechi baina ya Homa Bay Combined dhidi ya Kisumu Combined mechi zote zikisakatwa katika uwanja Jomo Kenyatta Mamboleo.

Wachezaji 22 bora kutoka kwa mashindano hayo watachuana na mabingwa wa Ligi kuu nchini Gor Mahia, kwenye fainali ya Jumamosi Disemba 30 katika uchanjaa wa Nyilima eneo la Asembo.

Mashindano hayo yanafadhiliwa na Waziri wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano na uchumi wa kidijitali Eliud Owalo.

Website |  + posts
Share This Article