Mifumo ya dijitali ya serikali: Kamati ya bunge yazua maswali

Dismas Otuke
1 Min Read

Kamati ya bunge la kitaifa ya Teknolojia ya Habari, Mawasiliano na Uvumbuzi chini ya usimamizi wa mbunge wa Dagoreti Kusini John Kiarie ilikutana na mamlaka ya ICTA Ikitaka kufahamishwa kuhusu maendeleo ya miradi ya mifumo ya kidijitali kama vile KDEAP, e-Citizen na intaneti ya umma yaani public Wi-Fi.

Kiarie alitaka kufahamu mpangilio na mikakati ya ICTA ya muda mrefu kuhusu miradi hiyo wakisisitiza umuhimu wa utoaji huduma za kidijitali kwa Wakenya wote na mamlaka hiyo ilivyo kisheria.

Mbunge huyo alitaka kufahamu kutoka kwa ICTA kuhusu ni nani aliyejukumiwa kuendesha mtandao wa e-Citizen na matumizi ya shilingi bilioni 3.5, ambazo KDEAP ilipokea kutoka kwa hazina kuu.

Akijibu, Afisa mkuu mtendaji wa ICTA Stanley Kamunguya alifafanua kuwa wanalenga kuboresha utoaji huduma akiongeza  kuwa walikabidhi majukumu yake kwa mamlaka ya mawasiliano nchini.

Kuhusu e-Citizen, Kamunguya alisema kuwa ilikabidhiwa serikali mwezi Januari mwaka 2023 chini ya usimamizi wa Mwanasheria Mkuu hadi Julai 2024 ilipokabidhiwa idara ya uhamiaji.

Share This Article