Miaka 25 tangu shambulizi la bomu katika ubalozi wa Marekani jijini Nairobi

Dismas Otuke
1 Min Read

Ni miaka 25 tangu kutekelezwa kwa mashambulizi ya bomu katika balozi za Marekani katika majiji ya Nairobi, Kenya na Dar es Salaam, Tanzania.

Jijini Nairobi, shambulizi hilo la Agosti 7 mwaka 1998 liliwaacha watu 5,000 wakiuguza majeraha huku wengine 213 wakiwemo raia 44 wa Marekani wakifariki.

Jijini Daresalaam, watu 11 waliangamia na wengine 4,000 kujeruhiwa.

Kama kumbukumbu, familia za waliopoteza wapendwa wao hufanya maombi na kuweka maua katika eneo la mkasa huo.

Balozi wa Marekani nchini Kenya Meg Whitman anatarajiwa kutoa hotuba ya kuwakumbuka wahasiriwa wa mkasa huo katika afisi za ubalozi huo leo Jumatatu saa tisa unusu alasiri.

Hata hivyo, familia za walioathirika bado zinalilia haki ya kulipwa ridhaa hadi wa leo huku wengi wakiachwa na ulemavu, mayatima na wajane.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *