Mhubiri afikishwa mahakamani kwa kumdhulumu mwanafunzi kimapenzi

Tom Mathinji
1 Min Read

Mhubiri mmoja katika eneo la Baringo kaskazini alifikishwa katika mahakama moja ya Kabarnet leo Jumanne, kwa makosa ya kumdhulumu kimapenzi na kumpachika mimba msichama wa umri wa maka 15.

Evans Bundotich, anadaiwa kuwa mnamo tarehe nne mwezi Disemba mwaka 2023, saa moja usiku katika kujiji cha  Tanyilel, alimdhulumu msichana huyo aliye katika kidato cha pili kwa maksudi.

Wakati huo huo, mshukiwa huyo anakabiliwa na kosa la pili la kushiriki mapenzi na mtoto, kinyume na sehemu ya 11 (1)  ya sheria za makosa ya ngono nambari tatu ya mwaka 2006.

Aidha mhubiri huyo pia alishatakiwa kwa kumpa dawa msichana huyo kwa lengo la kuavya mimba, kinyume na sheria.

Bundotich ambaye alifikishwa mbele ya hakimu mkuu Caroline Ateya, alikanusha mashitaka dhidi yake, akisema madai hayo si ya kweli.

Mahakama hiyo ilifahamishwa kuwa, mhubiri huyo hutembelea familia ya msichana huyo mara kwa mara, alienda kwa familia hiyo kutoa chakula cha msaada, kabla ya kutekeleza unyama huo.

Kiongozi wa mashtaka Vivian Ratemo, aliitaka mahakama kutomwachilia huru mshukiwa huyo, akidai kuwa maisha ya msichana huyo huenda yakawa hatarini.

Kesi hiyo itatajwa tarehe 12 mwezi Februari.

Share This Article