Mfumo wa kuweka kesi kidijitali wazinduliwa Mandera

Marion Bosire
1 Min Read

Jaji mkuu Martha Koome amezindua mfumo wa kuweka kesi mahakamani kwa njia ya kidijitali pamoja na kituo cha kusuluhisha mizozo almaarufu Maslaha. Alizindua pia sajili ndogo ya mahakama kuu katika kaunti hiyo ya Mandera.

Hii ni hatua kubwa katika eneo hilo katika mchakato wa kutafuta haki.

Mfumo huo wa kusajili kesi kidijitali unanuiwa kulainisha mchakato mzima wa kuweka kesi na taratibu za maombi kwa mahakama, kuimarisha ufuatiliaji kesi na kuimarisha matokeo kwa juma kwa watumizi wa mahakama na wahudumu wa mahakama.

Jaji mkuu Koome alisisitiza kwamba idara ya mahakama imejitolea kuhakikisha kwamba mifumo ya kupata haki imefikishwa karibu kabisa na wakenya.

Alisema pia kwamba njia za jadi za kusuluhusha mizozo hata kama ni muhimu, sio za pekee katika kuafikia haki.

Mifumo mbadala ya haki au “Alternative Justice Systems” inatarajiwa kufikika kwa urahisi, ya bei nafuu, iliyozoeleka na isiyo na urasimu mwingi na hivyo kuifanya kuwa rahisi kwa watu wa mashinani kufikia.

Idara ya mahakama pia imefungua mahakama za hakimu katika maeneo ya Elwak na Takaba, mahakam za kadhi huko Lafey, Rhamu na Banissa.

Gavana Mohamed Khalif wa Mandera alishukuru idara ya mahakama akisema hatua inazochukua tayari zimesababisha athari chanya katika jamii.

Share This Article