Hali ya majonzi imetanda katika soko la Soy, eneo bunge la Likuyani, mpakani mwa kaunti za Kakamega na Uasin Gishu baada ya mfanyabiashara mmoja kuuawa na watu wasiojulikana.
Maiti ya Noah Wekesa, mwenye umri wa miaka ishirini na mitano, ambaye huendesha biashara ya kuonyesha filamu, iligunduliwa baada ya watoto waliokuwa wakicheza karibu na eneo lake la kibiashara kupata rungu na upanga uliojaa damu karibu na mlango wake kabla ya kumuarifu mzee wa mtaa wa eneo hilo.
Kisa hiki kimethibitishwa na chifu wa kata ya Likuyani, Boniventure Lugado.
Lugado amesema uchunguzi umeanzishwa kuhusiana na mauaji hayo.
Wakazi wamelalamikia kuendelea kuzorota kwa hali ya usalama katika soko hilo.