Mfalme Charles asikitikia dhuluma zilizotekelezwa dhidi ya Wakenya

Tom Mathinji, Radio Taifa and Radio Taifa
1 Min Read
Mfalme Charles wa tatu.

Mfalme Charles wa tatu ameelezea majuto na huzuni mkubwa kutokana na dhuluma zilizotekelezwa na serikali ya Uingereza dhidi ya wakenya wakati wa harakati za kupigania uhuru wa taifa hili.

Mfalme huyo akiandamana na malkia Camilla,alisema hayo wakati wa dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa na Rais William Ruto na Mama Rachel Ruto Jumanne jioni katika ikulu ya Nairobi.

Rais Ruto alimualika mfalme Charles na malkia wake kuzuru maeneo kadha nchini yenye mandharia ya kuvutia.

Wakati wa dhifa hiyo iliyohudhuriwa na kinara wa upinzani Raila Odinga, mfalme Charles alielezea ari yake ya kukutana na waathiriwa wa dhuluma hizo za kihistoria.

Alikariri umuhimu wa pande zote mbili kushughulikia dhuluma hizo za kihistoria kwa njia iliyowazi.

“Ni muhimu sana kwangu kukutana na baadhi ya wale maisha yao na jamii zao ziliathiriwa pakubwa na dhuluma hizo,” alisema Mfalme Charles.

Ziara hiyo ya kifalme hapa nchini, itaangazia jinsi Kenya na Uingereza zitashirikiana pamoja katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na kutoa fursa za ajira kwa vijana.

Website |  + posts
Share This Article