Meneja wa Jux amtakia mema kwenye ndoa

Meneja huyo aitwaye Swagg Daddy kwenye mitandao ya kijamii aamekuwa na Jux kwa miaka 15 sasa.

Marion Bosire
1 Min Read

Meneja wa mwanamuziki Juma Jux ambaye hujiita Swagg Daddy kwenye mitandao ya kijamii amemtakia mema anapoanza safari ya ndoa rasmi.

Swagg alichapisha picha inayomwonyesha yeye, Jux na mkewe siku yao ya ndoa na kuandika, “Ndugu yangu Jux unaingia kwa safari hii mpya ya ndoa. Naomba Mwenyezi Mungu awe nanyi, akufungulie milango ya baraka.”

Aliendelea kumsifia Jux akisema kwamba wamekuwa marafiki na washirika wa kikai kwa muda wa miaka 15 sasa na kamwe hawajawahi kugombana au kupishana.

“Heshima, uaminifu na utu vimetutangulia kabla ya chochote. Tumeanza kama marafiki, leo tuko kama ndugu wa damu! Dunia hii imejaa changamoto, hasa inapokuja kwenye kazi na pesa, lakini kwetu sisi utu umekuwa kipaumbele.” aliendelea kusema Swagg.

Alimshukuru Jux kwa kumwamini na kumpa nafasi kubwa katika maisha yake. “Kuwa meneja wako si kazi tu, ni dhamana kubwa sana. Wengi hawajui, lakini msanii hufuata ushauri wa meneja wake kwa asilimia 80-90, si tu kwenye muziki, bali hata kwenye maisha yake binafsi.” aliongeza.

Jux alifunga ndoa Ijumaa Februari 7, 2025 na mpenzi wake wa asili ya Nigeria Priscilla Ojo, ambaye sasa amepatiwa jina la kiisilamu ambalo ni Hadiza Mkambala.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *