Mechi za raundi ya 16 bora kuwania kombe la mataifa Afrika- AFCON ,zimebainika kufuatia kukamilika kwa michuano ya makundi.
Katika mechi za mwisho za makundi ya E na F Jumatano usiku ,Tunisia watimuliwa mashindanoni baada ya kutoka sare tasa na Afrika Kusini, wakishika mkia kwa pointi 2.
Bafana Bafana walimaliza wa pili kwa alama 4 nao Mali licha ta kutoka sare kappa dhidi ya Namibia waliongoza kwa alama 5.
Katika kundi F Atlas Lions kutoka Morocco waliibwaga Zambia goli moja kwa bila na kuongoza kwa pointi saba, wakati DR Congo wakichukuwa nafasi ta pili kwa pointi 3 baada ya kutoka sare tasa na Tanzania.
Kipute hicho kinachukua mapumziko ya siku mbili Alhamisi na Ijumaa, kabla ya kurejea Jumamosi kwa awamunya 16 bora kwa derby ya COSAFA kati ya Angola na Namibia na baadaye derby ya Afrika magharibi baina ya Cameroon na Nigeria.
Jumapill Equatorial Guinea watamenyana na Guinea nao Misri wakabane koo na DR Congo
Jumatatu Januari 29, Cape Verde watafungua ratiba dhidi ya Mauritania kabla ya mabingwa watetezi Senegal kuwajulia hali wenyeji Ivory Coast.
Mechi mbili za mwisho zitasakatwa Juamnne Mali wakizindua uhasama dhidi ya Burkina Faso na hatimaye Morocco wamalize udhia na Afrika Kusini.